Soma Na video jinsi UAE walivyotuma Chombo Mars leo wakitokea japan
Umoja wa Falme za Kiarabu imeweka historia kwa kutuma chombo chake katika sayari ya Mihiri yaani Mars baada ya kufanikiwa kukirusha kutokea nchini Japani.
Chombo chake cha Hope kimerushwa kwa roketi ya H2-A kutoka kituo cha anga za juu cha Tanegashima na huenda sasa hivi kimeshapita kilomita milioni 500 kikielekea kufanya utafiti kuhusu hali ya hewa na anga katika sayari ya Mahiri.
Majaribio mawili ya awali ya kurusha chombo hicho wiki jana yalilazimika kufutwa kwasababu ya hali mbaya ya hewa.
Kuwasili kwa chombo Hope Februari 2021 kumepangiwa kusadifiana na maadhimisho ya miaka 50 tangu kuundwa kwa Muungano wa Falme za Kiarabu.
Mheshimiwa Bi. Sarah Al Amiri, anayeongoza kikosi cha chombo Hope, alizungumzia faraja yake na furaha aliyonayo kuona chombo hicho kikipaa salama kwenye anga. Na kusema kwamba hali itakayoshuhudiwa nchini kwao Julai 20, ni sawa tu na Marekani wakati raia wake waliposhuhudia chombo Apollo 11 Moon kikitua miaka 51 iliyopita,
"Ilikuwa kichocheo kwa kizazi chote kilichotazama ikipaa na kuwa na ndoto kubwa zaidi," ameiambia BBC News.
"Leo hii ninafuraha sana kwamba watoto wa Emirates asubuhi ya Julai 20, wakiwa na mradi wao unaoendelea, wakijionea uhalisia mpya wa mambo, uwezekano mpya ulio wingi wa matumaini, unaowaruhusu kuchangia zaidi na kuwa na mchango mkubwa duniani."
Chombo cha UAE ni moja na vyombo vitatu vilivyokwenda kwenye sayari ya Mahiri mwezi huu.
Marekani na China zote zina ujumbe wao unaotaka kwenda kwenye sayari hiyo ambao uko katika hatua za mwisho za matayarisho.
Ujumbe wa Marekani unaotumia chombo kwa jina Perseverance, umetuma pongezi zao kwa Hope. "Nasubiri kwa hamu kuunga na nyinyi kwenye safari hii!" umeandika kupitia akaunti yao ya Twitter.
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Kwanini UAE inakwenda kwenye sayari ya Mahiri?
UAE ina ujuzi kidogo katika suala zima la kuunda chombo cha angani lakini wameamua kujaribu kitu ambacho Marekani, Urusi, Ulaya na India ndio nchi pekee zilizofanikiwa kufanya.
Lakini inazungumzia ndoto za raia wa Emirates kwamba wamechukua changamoto hii na kuamua kujaribu.
Wahandisi wao waliofunzwa na wataalamu wa Marekani, wametengeneza chombo cha kisasa zaidi ndani ya kipindi cha miezi sita tu - na setilaiti hii itakapofika kwenye sayari ya Mahiri inatarajiwa kuwasilisha sayansi mpya, ya kipekee, kuvumbua vitu vipya jinsi sayari hiyo inavyofanyakazi.
Hususan, wanasayansi wanafikiria kwamba inaweza kuongeza uelewa wa jinsi sayari ya Mahiri ilipoteza hewa nyingi na umuhimu mkubwa wa maji yake.
Chombo Hope kinachukuliwa kama matumaini makubwa - kitu ambacho kitavutia vijana wengi zaidi huko Emirates na eneo zima la Uarabuni kuchukua masomo ya sayansi shuleni na katika elimu ya juu.
Setilaiti hii ni moja ya miradi serikali ya UAE inasema inaashiria nia yake ya kuondoa nchi hiyo katika utegemezi wa mafuta na gesi ikilenga uchumi wenye kuegemea zaidi elimu siku za usoni.
Lakini tangu zamani linapokuja suala la sayari ya Mahiri hatari zake ni za juu. Nusu ya ujumbe wote uliotumwa kwenye sayari ya 'Nyekundu' yaani Mahiri umeishia kushindwa. Mkurugenzi wa chombo Hope, Omran Sharaf, anatambua hatari zilizopo lakini amesisitiza kwamba nchi yake iko sahihi katika kujaribu.
"Utafiti huu na maendeleo yake na kushindwa ni machaguo," ameiambia BBC News.
"Hata hivyo, kushindwa kuendelea kama nchi sio chaguo. Na cha muhimu zaidi hapa ni fursa na uwezo ambao UAE imepata kutoka kwa ujumbe juu, na elimu itakayoleta kwa nchi yake."
Ujumbe wa Hope utafanya nini kwenye Mars?
Ujumbe wa Emirates haukutaka kufika kwenye sayari nyekundu na kurejea na yale yale ambayo yameshakusanywa na wengine.
Kwahiyo, wakaamua kwenda kwa kamati ya ushauri ya shirika la anga za mbali la Marekani na kuulizia ni utafiti gani ambao unaweza kuwa na manufaa katika taarifa ambazo tayari zishapatikana kupitia utafiti wa awali.
Kamati hiyo ikaweka mapendekezo ambayo ni malengo ya timu ya Hope. Setilaiti ya UAE itatafiti vile sayari hiyo inavyofanya kazi, nishati inavyozunguka kuanzia chini hadi juu, kila wakati kwa siku nzima na misimu yote ya mwaka.
Pia itafuatilia mengine kama vile vumbi ambalo mara nyingi linachangua pakubwa joto la anga.
Pia kikosi hicho kitafuatilia tabia za atomi za hydrojeni na oksijeni juu ya anga.
Kuna hisia kwamba atomi hizo zinachangia pakubwa katika kahuribu anga la sayari ya Mars kutokana na chembe za nishati kutoka kwenye jua.
Hili linachangia historia ya kuwa sayari hiyo sasa hivi ina upungufu mkubwa wa maji yaliyokuwepo awali.
Ili kupata taarifa hizi, Hope itachukua mzunguko wa karibu wa ikweta ambao uko mbali wa kilomita 22,000 hadi 44,000 kutoka kwenye sayari.
"Matamanio yaliyopo ni kufuatilia kila kitu kinachotokea kwa siku kunakofanya mzungumo kuwa mkubwa kisha umbo la yai," ameelezea mkuu wa kikosi cha Hope, David Brain LASP.
"Kwa kuchaguo hayo, tutaweza kufahamu kuhusu volkeno kubwa katika mfumo wa jua kwasababu huwa unazunguka muda tofauti tofauti kwa siku.
"Tutapata picha kamili za Mars lakini kamera yetu inachuja, kwahiyo sayansi yote inahusisha picha za namna hiyo"
Dogoo
ReplyDelete